Ufunuo wa Yohana 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
Ufunuo wa Yohana 1 (Swahili) Revelation 1 (English)

Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; Ufunuo wa Yohana 1:1

This is the Revelation of Jesus Christ, which God gave him to show to his servants the things which must happen soon, which he sent and made known by his angel to his servant, John,

aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona. Ufunuo wa Yohana 1:2

who testified to God's word, and of the testimony of Jesus Christ, about everything that he saw.

Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Ufunuo wa Yohana 1:3

Blessed is he who reads and those who hear the words of the prophecy, and keep the things that are written in it, for the time is at hand.

Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi; Ufunuo wa Yohana 1:4

John, to the seven assemblies that are in Asia: Grace to you and peace, from God, who is and who was and who is to come; and from the seven Spirits who are before his throne;

tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, Ufunuo wa Yohana 1:5

and from Jesus Christ, the faithful witness, the firstborn of the dead, and the ruler of the kings of the earth. To him who loves us, and washed us from our sins by his blood;

na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina. Ufunuo wa Yohana 1:6

and he made us to be a Kingdom, priests to his God and Father; to him be the glory and the dominion forever and ever. Amen.

Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Ufunuo wa Yohana 1:7

Behold, he is coming with the clouds, and every eye will see him, including those who pierced him. All the tribes of the earth will mourn over him. Even so, Amen.

Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi. Ufunuo wa Yohana 1:8

"I am the Alpha and the Omega,{TR adds "the Beginning and the End"}" says the Lord God,{TR omits "God"} "who is and who was and who is to come, the Almighty."

Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu. Ufunuo wa Yohana 1:9

I John, your brother and partner with you in oppression, Kingdom, and perseverance in Christ Jesus, was on the isle that is called Patmos because of God's Word and the testimony of Jesus Christ.

Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu, Ufunuo wa Yohana 1:10

I was in the Spirit on the Lord's day, and I heard behind me a loud voice, like a trumpet

ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia. Ufunuo wa Yohana 1:11

saying, "{TR adds "I am the Alpha and the Omega, the First and the Last."}What you see, write in a book and send to the seven assemblies{TR adds "which are in Asia"}: to Ephesus, Smyrna, Pergamum, Thyatira, Sardis, Philadelphia, and to Laodicea."

Nikageuka niione ile sauti iliyosema nami. Na nilipogeuka, niliona vinara vya taa saba vya dhahabu; Ufunuo wa Yohana 1:12

I turned to see the voice that spoke with me. Having turned, I saw seven golden lampstands.

na katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini. Ufunuo wa Yohana 1:13

And among the lampstands was one like a son of man, clothed with a robe reaching down to his feet, and with a golden sash around his chest.

Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho yake kama mwali wa moto; Ufunuo wa Yohana 1:14

His head and his hair were white as white wool, like snow. His eyes were like a flame of fire.

na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi. Ufunuo wa Yohana 1:15

His feet were like burnished brass, as if it had been refined in a furnace. His voice was like the voice of many waters.

Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kuume; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake. Ufunuo wa Yohana 1:16

He had seven stars in his right hand. Out of his mouth proceeded a sharp two-edged sword. His face was like the sun shining at its brightest.

Nami nilipomwona, nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kuume juu yangu, akisema, Usiogope, Mimi ni wa kwanza na wa mwisho, Ufunuo wa Yohana 1:17

When I saw him, I fell at his feet like a dead man. He laid his right hand on me, saying, "Don't be afraid. I am the first and the last,

na aliye hai; nami nalikuwa nimekufa, na tazama, ni hai hata milele na milele. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu. Ufunuo wa Yohana 1:18

and the Living one. I was dead, and behold, I am alive forevermore. Amen. I have the keys of Death and of Hades.

Basi, uyaandike mambo hayo uliyoyaona, nayo yaliyopo, na yale yatakayokuwa baada ya hayo. Ufunuo wa Yohana 1:19

Write therefore the things which you have seen, and the things which are, and the things which will happen hereafter;

Siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na ya vile vinara saba vya dhahabu. Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni makanisa saba. Ufunuo wa Yohana 1:20

the mystery of the seven stars which you saw in my right hand, and the seven golden lampstands. The seven stars are the angels of the seven assemblies. The seven lampstands are seven assemblies.